Wednesday, October 31, 2012

BASI LA ABOOD NAMBA T 545 AZE LA KUTOKEA DAR KWENDA TUNDUMA LAPATA AJALI MAENEO YA SAE(MBILINYI) BAADA YA KUGONGANA NA KENTA LILILO SABABISHA AJALI HIYO, MMOJA AFARIKI HAPO HAPO!

 Basi la Abood


 Hivi ndivyo basi La Abood lilivyo pata ajali baada ya kugongana na Kenta

Baadhi ya Abiria wakiwa wanapata maelekezo kutoka kwa polisi
BASI LA ABOOD LENYE USAJILI WA NAMBA T 545 AZE LIMEPATA AJALI MAENEO YA SAE SEHEMU MAARUFU  KWA JINA LA KWA MBILINYI LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA. AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MIZIGO AINA YA SCANIA LIKIWA LIMETOKEA ZAMBIA KUELEKEA DAR WAKATI WA KUTAKA KUPISHANA NA BASI HILO, NA NDIPO GARI AINA YA KENTA IKAJITOKEZA NA KUJICHOMEKA BARABARANI NA KUSABABISHA AJALI HIYO.

KATIKA AJALI HIYO MTU MMOJA AMBAYE  ANAITWA CHALE KITELEKE AMBAYE PIA ALIKUWA NDIYE KONDA WA BASI HILO AMEFARIKI PAPO HAPO, PAMOJA NA MAJERUHI NANE AMBAO WAMEKIMBIZWA HOSPITALINI .
HABARI KAMILI ITAWAJIA KESHO BAADA YA KUPATA TAARIFA KUTOKA POLISI.

PICHA ZOTE NA: MBEYA YETU BLOG
Post a Comment