Saturday, June 28, 2014

MARCIO MAXIMO

http://api.ning.com/files/3QWN5yhdbad*V5J9Z5LXoyU9C1YTVF3ARcS-ZlArd17Iw3owr1m*DmjHowRQr048ZJABB9cF9ukZtJYjbfuCqnv0TYZxfQrl/maximo3.jpg
Mbrazil Marcio Maximo hakuwa na mahusiano mazuri na Juma Kaseja mwaka 2007 alipokuwa anaifundisha Taifa Stars, lakini sasa amesema kazi inatakiwa kundelea Yanga kama kawaida na kusahau yaliyopita.
KOCHA Mbrazil, Marcio Maximo na msaidizi wake Leonadro Neiva wanatarajia kuanza kazi rasmi jumatatu baada ya kumwanga wino kuitumika Yanga sc  kwa mkataba wa miaka miwili.
Jana Maximo na mwenzake Neiva walikuwa na mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya Yanga, makutano ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, jijini Dar es salaam ambapo walieleza malengo yao na kujibu maswali ya wanahabari.
Ulikuwa mkutano mzuri na muhimu kwa wanamichezo, kwasababu walikuwa na kiu ya kujua nini Maximo ataongea kwa mara ya kwanza baada ya kurudi nchini, safari hii ikiwa ni Yanga na sio majukumu ya kitaifa.
Moja ya mambo aliyosema Maximo ni kufurahia kurudi Tanzania, iliwasifu watanzania kwa kuwa wakarimu, wapenda mpira na akaahidi kufanya kazi kwa ueledi mkubwa.
Pili Maximo hakusita kutoa shukurani zake kwa viongozi wa Yanga kwasababu wamemuamini na kumpa nafasi hiyo muhimu. Alikiri kufuatwa kwa awamu tatu mfufulizo, lakini safari hii akaona bora akubali.
Kitu ambacho wengi walisubiri kusikia kutoka kwa Mbrazil huyu mwenye heshima kubwa nchini, nikiwemo mimi, ni mipango yake ya kuifanya Yanga kuwa bora.
Maximo alipata fursa ya kueleza mipango yake ambapo alisema anatarajia kuanza kazi moja kwa moja siku ya jumatatu pamoja na msaidizi wake Neiva kwa kushirikiana na kocha wa kikosi cha U-20.
Alisema ataanza na wachezaji waliopo na wachezaji wa kikosi cha U20 ambapo watakua wakifanya mazoezi pamoja.
“Natambua tuna wachezaji wengi katika timu za Taifa mbalimbali ikiwemo ya Tanzania (Taifa Stars), Uganda  (The Cranes) na Rwanda (Amavubi) ambao wapo wanayatumikia mataifa yao, na punde watakapomaliza majukumu hayo wataungana nasi kwa maandalizi”
Post a Comment