Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini Jaji Mstaafu Damian Lubuva
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jana, kulia ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida, Liana Hassan na kushoto ni Mkurugenzi wa
Manispaa ya Singida Joseph Mchina.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi
imeanza mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,kwa
kuwashirikisha kwa karibu waandishi wa habari hapa nchini.
Lengo la kuwashirikisha
waandishi wa habari ni kutokana na uwezo na hekima katika kupeleka
taarifa na kuhamasisha jamii na wananchi kwa ujumla kupitia vyombo vya
habari.
Hayo yamebainisha jana mjini
hapa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian
Lubuva wakati akifungua mkutano na waandishi wa habari wa Mkoa wa
Singida.
Jaji Lubuva alisema lengo ni
kuhakikisha kuwa wale wote wenye sifa za kuwa wapiga kura wanajitokeza
kwa wingi katika vituo vya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura.
Aidha alisema kuwa Tume
inatarajia kufanaya uboreshaji wa Daftari la Kudumu wa Wapiga kura kwa
awamu ya kwanza hivi karibuni kwa kutumia Teknolojia mpya ya Biometric
Vote Regstration ( BVR).
Alisema mfumo huo mpya ni wa
kuchukua au kupima taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu
na kuhifadhi katika kanzi data kwa ajili ya utambuzi.
“Mfumo huu hutumika katika
kumtambua mtu na kumtofautisha na mwingine, ingawa tabia hizo za
binadamu ziko nyingi, lakini kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura alama
za vidole kumi vya mikono, picha na saini ndizo zitachukuliwa na
kuhifadhiwa kwenye Kanzi Data (Database) ya wapiga kura.” Alisisitiza
Jaji Lubuva.
Hata hivyo alisema kwa kutumia
mfumo huu wa (BVR), wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale
walio na kadi za mpiga kura watatakiwa kuandikishwa upya.
Jaji Lubuva alisema mafunzo kwa
Watendaji yanatarajiwa kufanyika muda kuanzia Mwezi Julai mwaka hauu
kabla ya zoezi la uboreshaji wa Daftari kufanyiaka.
Mwenyekiti huyo alibainisha
kwamba uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura umeshafanyika na kwa
sasa uandikishaji utafanyika katika vituo vilivyo katika ngazi ya
vitongoji, Vijiji na Mitaa.
“ Kutokana na utaratibu huu wa
sasa vituo vya kujiandikisha vimeongezeka kutoka 24,919 hadi kufikia
vituo 40,015 ambavyo vimewekwa katika ngazi za Vitongoji, Vijiji na
Mitaa’. Alisema na kuongeza
“Ili kuwezesha kuwa karibu
zaidi na wanancahi na hivyo kupunguza malalamiko ya auambali wa vituo
vya kujiandikisha na kuaongeza mwamko wa kujiandikishwa na kupiga kura.”
Alifafanua Jaji Lubuva.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Manispaa ya Singida, Joseph Mchina, alisema maandalizi yote muhimu kwa
ajili ya zoezi hilo katika Manispaa yake yamekamilika na hivyo kuwa na
vituo 154 badala ya 84 vya awali.
No comments:
Post a Comment