Wednesday, November 26, 2014

MAANDALIZI YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA YAKAMILIKA KUFANYIKA DISEMBA 14-2014

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo. Kushoto ni  Mkurugenzi Msaidizi Idara za Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Denis Bandisa.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (Tamisemi), Jumanne Sagini (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo. 
 Mkurugenzi Msaidizi Idara za Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Denis Bandisa, akiwaonesha wanahabari daftari la kura wakati akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo kuchukua taarifa hiyo.
 
 Na -Dotto Mwaibale
 
WAKATI wananchi wakijishauri kujiandikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (Tamisemi ) imekiri kuzorota kwa zoezi hilo,na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
 
Akizungumza na waandishi wahabari Dar es salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Jumanne Sagini alisema kuzorota huko kumetokana na serikali kuchelewa kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kusababisha kukosa muelekeo.
 
Alifafanua kuwa kwa kawaida uchaguzi huo hufanyika mwezi oktoba na hivyo waziri mkuu anatakiwa kutoa taarifa hiyo siku 30 kabla lakini kutokana na kuwepo kwa bunge lakatiba hali hiyo ilibadilika na hivyo kuiilazimu serikali kusogeza mbele mchakato huo.
 
“Nikweli hali hiyo ipo kama mnavyosema wandishi,lakini nyie ndio mnatakiwa kutusaidia kuzidi kutoa elimu,tumekuwa tukifanya vipindi katika vyombo mbalimbali vya habari lakini bado elimu inahitajika zaidi”alisema.
 
“Na wiki ya kwanza jambo hili lilionekana kuzorota kwa sababu ilikuwa ni wiki ya wagombea kuchukua fomu,wananchi wakajua ni siku ya kujiandikisha,lakini mchakato unakwenda vizuri kwasiku hizi mbili”aliongeza.
 
Sagini alipoulizwa na wandishi kuhusu mkanganyiko wa vituo vya kupigia kura alisema vituo vyoye vilivyopo katika mazingira ya huduma za Afya zinatakiwa kuondolewa na kupelekwa kwenye shule za msingi ilikuepusha usumbufu kwa kwa wagonjwa.
 
kauli hiyo ilitokana na kuwepo kwa kituo cha Zahanati ya Tandale kugeuzwa kuwa kituo cha uandikishaji kwa wapiga kura hali inayopeleka wagonjwa kulalamika kuwa wanapata usumbufu,hivyo kuwataka wahusika kuhamisha kituo hicho.
 
 
Akizungumzia bajeti ya uchaguzi huo, Mratibu wa uchaguzi Taifa, Denis Bandisa alisema serikali imetenga bilioni 20 kwa ajili ya uchaguzi huo ambapo,kati ya hizo bilioni nane kwa ajili ya malipo ya makarani,bilioni sita vifaa vya kujiandikishia,na bilioni sita kwa ajili ya matumizi mengine.
 
Hata hivyo Denis hakutaka kubainisha kuwa matumizi mengine ni yapi katika fedha hizo,na kusema kila karani atakuwa atalipwa sh. 10,000 kwa siku kutokana bajeti ya serikali kuwa ndogo.
 
“Kipindi cha mwanzo tlikuwa hatulipi kabisa,kwasababu sio kazi ngumu,ila kwasasa tukaona sio vema kwa sababu wanatumia nauri zao,tukaamua kutenga kiasi hicho cha fedha ila badae tutaangalia utaratibu wa kuwaongezea katika uchaguzi mkuu”alisema Denis.
 
Hata hivyo alitaja idadi ya kata zinazo husika na uchaguzi kuwa ni 3,802,mitaa 3741,Vijiji 12,443 na vitongoji 64,616.
 
Hata hivyo gazeti hili lilipa baadhi ya vituo na kushuhudia makarani wakisema kuwa kwasiku huandikisha wananchi 30.
Post a Comment