Tuesday, November 11, 2014

PROFESA JOHN NKOMA AWAFUNDA MABLOGGER JINSI YA KUANDIKA KWA USAWA HABARI ZA UCHAGUZI

1Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania TCRA Profesa John Nkoma akizungumza katika mkutano na Mablogger wakati alipofungua mkutano huo uliojadili jinsi ya kuripoti kwa usawa habari za uchaguzi wa serikali za mitaa, Ubunge na Rais kuanzia mwaka huu mpaka mwakani, Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo pia viongozi wa Muda wa kuratibu uanzishwaji wa  Chama cha Mablogger wamechaguliwa ambao ni Joachim Mushi, Aron Msigwa mwakilishi kutoka serikalini, Shamimu Mwasha Blog za Biashara, Francis Godwin mablogger wa mikoani, Othman Maulid mwakilishi kutoka Zanzibar, Khadija Khalili, William Malecela na Henry Mdimu ambao wataongoza kwa muda wakati wa mchakato huo mkutano huo umesimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano TCRADSC_5572Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene akifunga rasmi mkutano huo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.10 
Baadhi ya Malogger wakiwa katika mkutano huo. 9 
Kutoka kushoto ni Josephat Lukaza wa Lukaza Blog, Shamimu Mwasha wa 8020Fashion na Geofrey Wapamoja Blog wakiwa katika mkutano huo 8 
Baadhi ya maofisa kutoka TCRA wakiwa katika mkutano huo.  6 
John Bukuku Mkurugenzi wa Fullshangweblog.com akiwa katika mkutano huo. 5
Baadhi maofisa wa TCRAwakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano  4 
Andrew Kisaka Ofisa Mwanamizi wa Utangazaji TCRA akitoa mada katikamkutano huo.

No comments: