Monday, November 10, 2014

Rais Kikwete afanyiwa upasuaji wa tezi dume Marekani, hali yake inaendelea vyema

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akizungumza na  Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya
Johns Hopkins na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi(kulia) baada
ya kuwasili katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore,
Maryland,  Marekani kwa upasuaji Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo
uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.(Picha na Fred Maro) unnamed2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa
Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha
upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo
Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua
muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
…………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa
upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji
matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa
Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini
ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete
kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
DAR ES SALAAM,

No comments: