Saturday, November 1, 2014

TANZANIA NA BURUNDI ZA SAINI MKATABA WA MIAKA 50 KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA MRADI WA RUSUMO

 Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa, 
Sospeter Muhongo.
 Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, 
Come Manirakiza.
 Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Come Manirakiza wakisaini mkataba huo.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto), akibadilishana hati na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Come Manirakiza, baada ya kutiliana saini mkataba wa miaka 50 wa  usafirishaji wa umeme kutoka Mradi wa Rusumo kwenda nchini humo katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Mradi huo unazihusisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
Hapa mkutano wa maofisa wa Tanaznia na Burundi ukiendelea.
 Maofisa wa Tanzania wakiwa kwenye hafla hiyo ya 
kusaini mkataba huo.
 Maofisa wa Burundi na Tanzania wakiwa katika 
hafla hiyo.
 Maofisa wa Burundi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
 Maofisa wa Tanzania wakiwa kwenye tukio hilo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania , Profesa, Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati na Madini wa nchi ya Burundi, Come Manirakiza wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa nchi hizo mbili wanahusika na wizara hiyo.
 
SERIKALI ya Tanzania na Burundi zimesaini mkataba wa miaka 50 wamakubaliano wa mradi wa pili wa kusafirisha umeme utakaozalishwa kwenye kituo cha Rusumo.
 
TANZANIA NA BURUNDI ZA SAINI MKATABA WA MIAKA 50 KUSAFIRISHA UMEME KUTOKA MRADI WA RUSUMO
Awali Tanzania, Burundi na Rwanda zilisaini mkataba wa kwanza wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme cha rusumo chenye mega watt 80, kilichopo wilayani Ngara, Mkoani Kagera, mwaka 2013 ambacho kiligharimu takribani dola za kimarekani milioni 340 zilizotolewa na benki ya Dunia.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kusaini mkataba huo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo, alisema mkataba huo umezihusisha nchi mbili ambapo alibainisha kuwa kupitia mradi huo ambao umeanza katika sehemu ya mwisho ya kutekeleza mradi wa kwanza ulioanza mwaka jana yapo baadhi ya maeneo nchini yatapata umeme.
 
Alisema kupitia mradi huo nchi itaweza kuimarisha grid ya Taifa na kupunguza tatizo la umeme kwenye maeneo mengi nchini.
 
Waziri Muhongo aliongeza kuwa pamoja na hatua hiyo pia kuitia mradi huo utaajiri wafanyakazi kutoka nchi zote tatu na hata wa mataifa mwengine ambapo alibainisha kuwa kwa sasa katika kituo cha mto rusumo wapo walioajiriwa kutoka nchi husika na miradi hiyo na mataifa mengine.
 
Kuhusu ujenzi wa mfumo wa usafirishaji umeme alisema kila nchi itajitegemea katika kusafirisha umeme na kubainisha kuwa Tanzania itajenga mfumo huo kuanzia miaka michache ijayo.
 
Hata hivyo Prof. Muhongo hakubainisha kiasi halisi kitakacho tumika kuendeshea mradi huo wa wamu ya pili

No comments: