Thursday, December 11, 2014

Baada ya kutua DSM Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan alonga na wanahabari

 Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo,wakati akizungumzia ushindi wake na uzoefu alioupata katika Jumba hilo la Big Brother huko nchini Afrika Kusini.Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi.
  Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
Idris akizungumza.
 Alikuwa Mshiriki mwenza wa Idris Sultan,Irene Laveda akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi akizungumza jambo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo.
 Sehemu ya Waandishi wa habari waliofika katika Hoteli ya Hyatt Regency kumsikiliza Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan.
Mshindi wa Big Brother 2014,Idris Sultan (pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Furaha Samalu (pili kulia),Meneja Uhusiano wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) pamoja na Mwanalibeneke
 Wadau wakipiga picha ya pamoja na Idris na Laveda.

Na   Bakari   Issa,Dar  es  Salaam
 
Mshindi  wa  Big  Brother  Africa   2014,Idris  Sultan ameeleza  siri  ya mafanikio yake  katika  shindano lililomalizika hivi karibuni  nchini  Afrika   ya  Kusini mbele ya waandishi wa habari waliofika kumsikiliza leo kwenye hoteli  ya  Hyatt Regency jijini  Dar  es  Salaam.
 
Idris  alifanikiwa kupata  ushindi  huo  baada  ya  kupigiwa kura  na nchi tano ambazo   ni  Tanzania,Kenya,Uganda,Rwanda pamoja na Namibia  na  kutwaa  Dola  za  Kimarekani 300,000  sawa  na  shilingi  Milioni 500 za Kitanzania na kufanikiwa kumbwaga mpinzani wake,Tayo kutoka  nchini Nigeria.
 
Idris  amesema  kuwa  ushindi   huo  ni  kwa  ajili  ya  mashabiki  hususan   waliompigia  kura  wakati  akiwa  katika  jumba   la  Big  Brother  huko  Afrika  ya  Kusini  na  kutoa  shukrani  kwa  nguvu,bidii  ambazo  watu  walimuekea  yeye na  kupata  ushindi  huo.
 
“Ushindi huu si wa kwangu peke yangu bali ni ushindi wa mashabiki ambao waliniwekea nguvu  pamoja na bidii na kufanikisha ushindi huu,”alisema Idris.
 
Pia  Idris  amezitaja  changamoto  alizokutana nazo  katika  jumba  la  Big  Brother  kuwa ni  kutokumjua mtu kama anakurekebisha au anakutoa kwenye njia,hivyo basi kushindwa kujua njia  sahihi ya kushindana.
 
“Kutokujua Waafrika wanafikiriaje, hauwezi   kujua    mtu    anakurekebisha     au  anakupotosha au  anakutoa  kwenye  njia,unashindwa kufahamu hiyo ndiyo changamoto niliokutana nayo,”alieleza  Idris
 
Aidha, amewataka  washiriki wa Tanzania watakaokuja kushirika shindano hilo,wasifikirie watu  wanafanya nini ndani ya jumba bali wafanye wao kama wao na sio kumuiga mtu mwingine.

No comments: