Monday, December 8, 2014

Kwenye Mashaka, Ni Heri Kumwacha Mtu Huru Kuliko Kumtia Hatiani..



Ndugu zangu,
CAG wetu mpya alitamka jambo la msingi sana akiwa Arusha hivi karibuni. Kwamba kuna tatizo la migongano ya kimaslahi kwenye kuyashughulikia matatizo yetu.

Ona leo, tayari tunayaona mapungufu makubwa kwenye hata ripoti za kichunguzi zilizowasilishwa Bungeni hivi karibuni. Kwamba kwa baadhi ya waliohusika kufanya uchunguzi wameonekana kuwa na migongano ya kimaslahi kwenye walichokichunguza na kukitolea taarifa.

Kama ilivyomshangaza Jaji Warioba, kuna wengi wanaoshangazwa, kuwa iweje wahusika wengine kwenye kuhusiana na kashfa ile ya Tegeta Escrow hawakuainishwa kwenye ripoti na wala hayakutoka maazimio ya hatua za kuchukuliwa dhidi yao.

Na juzi tu, tumesikia, kuwa viongozi wa kidini waliotuhumiwa ' wamesafishwa' kwa dhambi ile ile ambayo viongozi wa kisiasa wametuhumiwa na kuhukumiwa nayo.
Kauli ya CAG Assad ilikuwa ni thabiti na ya kuzingatiwa sana. Vinginevyo, kwenye mashaka, ni heri kumwacha huru mtu kuliko kumtia hatiani.

Maggid,
Iringa. 

No comments: