Tuesday, December 16, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,

WATU WATANO WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.143 AJR AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ROBERT MWAKIBIBI (37) MKAZI WA UYOLE KUACHA NJIA NA KISHA KUPINDUKA KATIKA ENEO LA KIJIJI CHA KANTELA WILAYA YA RUNGWE.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.12.2014 MAJIRA YA SAA 11:45 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANTELA-NTOKELA, KATA YA NTOKELA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.
WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI WANAWAKE WATATU NA WANAUME WAWILI AMBAO NI 1. SOPHIA OMARY (50) MKAZI WA MBALIZI 2. STELA MWALUSWASWA (38) MKAZI WA TUNDUMA 3. SUZANA MELELE (31) MKAZI WA MBALIZI 4. BULELE MWAIPAJA (48) MKAZI WA UYOLE NA 5. JACOB NYALUKE (17) MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI MBOZI MISHENI NA MKAZI WA MBOZI.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 32 WALIJERUHIWA KATI YAO WANAUME NI 16 NA WANAWAKE NI 16 AMBAO WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI ZA MISHENI IGOGWE NA MAKANDANA – TUKUYU. CHANZO CHA AJAIL NI HITILAFU KATIKA MFUMO WA BREKI WA GARI HILO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment