Sunday, March 22, 2015

WAZIRI LUKUVI AFUNGUA NYUMBA ZA NHC MRARA BABATI

1
Sehemu ya nyumba 40 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati mkoani Manyara ambazo zilifumguliwa rasmi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
……………………………….
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi amehitimisha ziara yake ya kutatua migogoro ya Ardhi katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Manyara na ameweza pia kuweka jiwe la msingi mradi wa nyumba za gharama nafuu Buswelu Mwanza na kufungua nyumba za aina hiyo zilizojengwa na NHC katika eneo la Longido Arusha na Mrara Babati. Picha za ufunguzi wa Mradi wa Mrara na Muungano Saguya-Babati
New Picture (1)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo kwa watendaji wake muda mfupi kabla ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati mkoani Manyara
New Picture (2)
Kikundi cha sanaa kikiburudisha halaiki ya wananchi( haiku pichani) iliyohudhuria ufunguzi uliofanywa na Waziri Lukuvi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati mkoani Manyara.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akionyeshwa mipaka ya eneo linalomilikiwa na NHC na Msimamizi wa Mradi wa NHC Mrara Babati Bi Linda Kasilima baada Mkurugenzi Mkuu kubaini kuwepo kwa uvamizi wa baadhi ya viwanja vya Shirika. Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ameagiza wote waliovamia viwanja hivyo kunyang’anywa mara moja na nyumba zao kuvunjwa bila fidia.
New Picture (4)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili katika mradi wa nyumba za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC ambapo aliifungua rasmi baada ya kukamilika. Nyjmba hizo 40 sasa zinauzwa kwa wananchi mbalimbali wa Babati na nje ya Wilaya hiyo wanaohitaji.
New Picture (5)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akivishwa skafu na skauti kuashiria alama ya amani, upendo na mshikamano mara alipowasili kufungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la rara Babati.
New Picture (6)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitambulishwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati Bi. Linda Kasilima alipowasili kufungua rasmi nyumba hizo.
New Picture (7)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati. Nyumba hizo zimeshakamilika na zinauzwa kwa wananchi wanaohitaji wa Bbati na nje ya Babati.
New Picture (8)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kufungua nyumba iliyotayarishwa kuwakilisha ufunguzi rasmi wa nyumba 40 za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Nkaya Bendera, Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jituson Vrajilal na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu .
New Picture (9)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoka katika nyumba ya mfano aliyoifungua baada kukagua vyumba na ubora wa nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
New Picture (10)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo ya mradi kwa Mhe. Waziri wa Ardhi na halaiki ya wananchi wa Babati(hawapo pichani) waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
New Picture (11)
Sehemu ya halaiki ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
New Picture (12)
Mkuu wa Wilaya ya Babati Bw. Crispin Meela akisalimia wananchi na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manayara kusalimia wananchi katika sherehe za ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
New Picture (13)
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera akihutubia wananchi na kusisitiza maafisa ardhi na mipango miji kufuata sheria katika usimamaizi na utoaji haki za ardhi Mkoani humo wakati wa sherehe za ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
New Picture (14)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akihutubia wananchi na kusisitiza Halmashauri za Wilaya kutenga ardhi kwa ajili ya kuwezesha NHC kujenga nyumba nafuu alipofungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
New Picture (15)
Mbunge wa Babati Vijini Mhe. Mhe. Jituson Vrajilal akitoa neon la shukrani kwa NHC kwa kuwezesha Wilaya ya Babati kupata nyumba bora na kusaidia vijana mashine za kufyatulia matofali huku akichagiza VETA na taasisi zingine zihusike kusaidia vijana.
New Picture (16)
Mbunge wa Viti maalum Paulina Gekul akisalimia wananchi na kumpongeza Waziri Lukuvi kwa kuacha ofisi ili kusikiliza kero za wananchi hali aliyosema inafaa kuigwa na Mawaziri wengine.

No comments: