Friday, April 3, 2015

WITO WA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA WAKAZI WA MKOA WA MBEYA KUELEKEA PASAKA.


download (2) 
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWATAKA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MBEYA KUSHEREKEA KWA AMANI SIKUKUU YA PASAKA BILA KUWEPO KWA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI
ZIPO KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA ZA NYUMBA ZA IBADA, TUNAPENDA KUWAKUMBUSHA VIONGOZI WA NYUMBA HIZO ZA IBADA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA NYUMBA HIZO, WAUMINI NA MALI ZAO KAMA VILE VYOMBO VYAO VYA USAFIRI WAKATI WA IBADA ZA MKESHA WA PASAKA.
KWA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE, TUNAWAKUMBUSHA KUWEKA WALINZI WA NDANI YA UKUMBI, KUZINGATIA MUDA WA KUANZA NA KUFUNGA KUMBI ZAO PAMOJA NA KUZINGATIA UWEZO WA UKUMBI UKILINGANISHA NA IDADI YA WATU.
KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO WAWE MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI. KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KAMA VILE WATEMBEA KWA MIGUU, WAENDESHA BAISKELI NA WASUKUMA MIKOKOTE KUWA MAKINI KATIKA MATUMIZI YA BARABARA IKIWA NI PAMOJA NA KUVUKA MAENEO RASMI YA KUVUKIA PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA.
PIA JESHI LA POLISI LINAWAKUMBUSHA WAZAZI NA WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO KATIKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU IKIWA NI PAMOJA NA KUHAKIKISHA MTOTO ANAKUWA CHINI YA UANGALIZI WA MTU MZIMA WAKATI WA KUTOKA NYUMBANI KUELEKEA NYUMBA YA IBADA AU MAENEO YA SHEREHE. KUHUSU DISCO TOTO, HATURUHUSU WATOTO KUCHEZA MUZIKI KATIKA KUMBI NA NI VYEMA WAKACHEZA KWENYE MAENEO YALIYOWAZI KWA AJILI YA USALAMA WAO. PIA TUNASHAURI WANANCHI, KUACHA WAANGALIZI KATIKA NYUMBA ZAO WANAPOTOKA KUELEKEA KATIKA IBADA AU SEHEMU ZA STAREHE ILI KUEPUKA MATUKIO YA UVUNJAJI, WIZI, UDOKOZI NA UPOTEVU WA MALI.
KWA UPANDE WA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA, TUMEJIPANDA VYEMA KUFANYA DORIA ZA MIGUU, MAGARI, NA PIKIPIKI KATIKA MAENEO YOTE KUZUNGUKA JIJI LA MBEYA NA VIUNGA VYAKE. PIA KWA KUSHIRIKIA NA KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA ZA NYUMBA ZA IBADA, PIA TUMEZITAMBUA NYUMBA ZA IBADA ZITAKAZOFANYA IBADA ZA MKESHA WA PASAKA NA TUTAWEKA ASKARI KATIKA NYUMBA HIZO KWA KUSHIRIKIANA KUFANYA KAZI PAMOJA NA KAMATI HIZO HASA KATIKA IBADA ZA MKESHA WA PASAKA. PIA ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WATAKUWEPO KATIKA MAENEO YOTE KUHAKIKISHA USALAMA WA WATUMIAJI WA BARABARA NA KUDHIBITI MADEREVA WASIOFUATA NA KUTII SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
AIDHA TUNAPENDA KUWAAMBIA WANANCHI WAZINGATIE USEMI HUU “USALAMA KWANZA, KWANI MAHALI POPOTE PENYE USALAMA, AMANI NA UTULIVU NDIPO MAENDELEO YA ENEO HUSIKA YANAKUWEPO. BILA USALAMA, HUTOWEZA KWENDA KUABUDU KWENYE NYUMBA ZA IBADA, HUTOWEZA KWENDA KULIMA, HUTOWEZA KUFANYA BIASHARA, KWENDA HOSPITALINI KUTIBU AU KUTIBIWA, KUSAFIRI BILA HOFU NAKADHALIKA. KWA MAANA HIYO, USALAMA NI KITU CHA MUHIMU KWA MAENDELEO YA MAISHA YETU, MKOA WETU NA TAIFA LETU.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA PASAKA YENYE AMANI NA UTULIVU.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: