Friday, May 1, 2015

WAFANYAKAZI WAHIMIZWA KUJITOKEA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE BIBI ZAINABU MBUSSI AKIONGEA NA WAFANYAKAZI WA WILAYA YA RUNGWE NA WANANCHI WALIOJITOKEZA KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIA ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA TUKUYU MJINI

BWANA EDIGA MYAVANU AKIWA NI MMOJA WA WAFANYA KAZI BORA WA MWAKA AKIPATA ZAWADI YA CHETI KUTOKA KWA MKUU WA WILAYA ZAINABU MBUSSI

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA AKIPOKEA MAGODORO YALIYOTOLEWA NA UMOJA WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI WILAYANI RUNGWE UKIWA NI MCHANO WA KIJAMII KWA WAFUNGWA KATIKA GEREZA LA TUKUYU MJINI



AFISA MICHEZO NA UTAMADUNI WILAYA YA RUNGWE MWL ENZ SEME AKIONGOZA RATIBA KATIKA SIKU YA WAFANYAKAZI WILAYANI RUNGWE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.

Hayo yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe kuhamasisha wafanyakazi.

Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
 Wafanyakazi wa Tume ya Uchaguzi (NEC) wakiwa katika maandamano kusherekea siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI huku wakiwa na bango lenye ujumbe wao mahususi kuwahamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha na wapige kura kuchagua kiongozi bora.
 Wafanyakazi wa Mamlaka  ya anga nao  hawakuwa nyuma na mabango yao.
 Wafanyakazi wa Ofsi ya Rais – Ikulu…
 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege ya Air Tanzania…
Mabango mbalimbali yamebeba kaulimbiu juu ya kuhamasisha wafanyakazi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura km. Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa wa Zamani (Picha na Christina Njovu).

No comments: