Saturday, June 13, 2015

Apple yazindua programu ya muziki


Kampuni ya Apple imetangaza kubuni programu tumizi mpya inayojumuisha maktaba ya kupeperusha muziki moja kwa moja kwenye internet, programu ya kusikiliza redio kwenye intaneti na njia maalum ambayo wasanii wataweza kubadilishana vibao vya miziki ambayo bado haijachapishwa rasmi.
App hiyo mpya inajumuisha mfumo wa kubashiri na kupendekeza utakaotumia mwelekezo wa binadamu kuchagua pamoja na sheria ya hisabati ya kutegua kitendawili kwa mifumo au algorithms.
App hiyo mpya inalenga kuzipa upinzani Spotify, Tidal na app nyinginezo za muziki. Kwa habari hizi na zingine za teknolojia tazama makala ya wiki hii ya Click.(Muro)
Post a Comment