Saturday, June 13, 2015

JK aongoza maadhimisho ya siku ya watu wenye Albinism Duniani leo jijini Arusha.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na baadhi ya watoto wenye albinism mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo wa Sheikh amri Abeid mjini Arusha leo ambapo aliongoza maadhimisho ya siku ya watu wenye Albinism Duniani leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na baadhi ya watoto wenye albism katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha wakati wa maadhimisho ya siku ya watu wenye albinism Duniani leo. Picha na Freddy Maro.(Muro)
Mwenyekiti wa Chama Cha Albino Tanzania Bwana Ernest Kimaya akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) muda mfupi baada ya kuwasili jana jioni.Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa wa Albino itakayofanyika leo katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid. Kushoto ni Bwana Godson Mollel mwenyekiti wa Chama cha Albino Mkoa wa Arusha. Picha na Freddy Maro.(Muro)

No comments: