Friday, June 12, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KARAGWE MKOANI KAGERA, KESHO KUENDELEA KYERWA

32
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mji wa Kayanga kwenye uwanja wa Kayanga wilayani Karagwe akiwa katika ziara yake ya kikazi ya mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza yenye lengo la kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KARAGWE)
31 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumzia suala la wakulima wa kahawa mkoani Kagera ambao wamekuwa wakipunjwa kutokana na bei ndogo ya zao la kahawa ukilinganisha na Uganda jambo ambalo linatokana na kodi nyingi zilizowekwa kwenye zao la kahawa nchini Tanzania ambazo zote zinaenda kumuangukia mkulima.
30
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa Kayanga wilayani Karagwe.
29
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.
28
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisisitiza jambo katika mkutano huo.
27
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aukiwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nyaishozi.
26
Mmoja wa wasanii akipiga ngoma wakati wa mapokezi ya Kinana katika kijiji cha Kaishozi
25
Wafanyakazi wa kampuni inayojenga barabara ya Kyaka -Begene wilayani Karagwe wakiendelea na kazi wakati Kinana alipokagua ujenzi wa barabara hiyo iliyokamilika kwa asilimia 85%.
24
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa barabara ya Kyaka -Begene wilayani Karagwe.
21
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella katikati, Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mh Deodatus Kinawiro kulia na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera mama Costansia Buhie ni miongoni mwa viongozi wa mkoa wa Kagera walioambatana  na Kinana katika ziara hiyo.
19
Kinana akisalimiana na Deodatus Kinawiro Mkuu wa wilaya ya Karagwe mara baada ya kuwasili wilayani humo.
18
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akishuka kwenye mtambo mkubwa wa kisawazisha mashamba ya miwa katika kiwanda cha Kagera Sugar wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua utayarishaji wa mashamba hayo.
17
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishuka kwenye mtambo mkubwa wa kisawazisha mashamba ya miwa katika kiwanda cha Kagera Sugar wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua utayarishaji wa mashamba hayo.
16
Moja ya Mitambo hiyo ukiwa umeegeshwa tayari kwa kazi ya kusawazisha mashamba hayo.
15
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha  mtambo mkubwa wa kisawazisha mashamba ya miwa katika kiwanda cha Kagera Sugar wakati  alipokagua utayarishaji wa mashamba hayo.
14
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mtaalam wa kilimo Bw. Chriss Davis wakati alipokagua utayarishaji wa mashamba ya miwa katika kiwanda cha Kagera Sugar mkoani Kagera.
13
Kazi ikiendelea.
12
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wataalam mbalimbali wa kilimo katika mashamba ya miwa ya kiwanda cha Kagera Sugar mkoani Kagera.
11
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Kagera Sugar wakati alipokagua mitambo ya kusukuma maji iliyojengwa kandokando ya mto Kagera ambayo inatumika kumwagilia miwa wa pili kutoka kushoto ni Nassir Seif Mkurugenzi wa kiwanda hicho na wa pili kutoka kulia ni Ashwin Rana Meneja Mkuu, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella.
10
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mitambo hiyo  jinsi inavyofanya kazi.
9
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wataalamu mbalimbali wanaoendesha mitambo ya kilimo cha umwagiliaji katika mashamba ya miwa ya kiwanda cha Kagera Sugar, kulia ni Mbunge wa Nkenge mama Asumpta Mshama.
8
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Meneja mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar Bw.Ashwin Rana wakati akitembelea kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar kushoto ni John Mongella Mkuu wa mkoa wa Kagera.
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wataalamu wa uzalishaji katika kiwanda cha Kagera Sugar wakati alipotembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji na changamoto mbalimbali zinazokabili kiwanda hicho.
6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Meneja mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar Bw.Ashwin Rana wakati akitembelea kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar
4
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. John Mongella akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yaliyofanyika kiwandani hapo wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanda hicho.
3
Meneja mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar Bw.Ashwin Rana akiwasilisha mambo kadhaa wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea kiwanda cha Kagera Sugar mkoani Kagera.
1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na  wakati na kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano na Bw. Ashwin Rana Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari Kagera Sugar.
Post a Comment