Napenda
kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada
Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye, na migu yake iliyopooza)
mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi
na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa
miaka 4.
Kwa
bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa
na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema
alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako inasemekana
alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.
Katika
uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,
hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada
ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa shilingi
550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi
nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani
kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya
wazazi wote wawili kufariki dunia.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo
nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa
kumpata daktari bingwa wa mifupa . Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze
process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital hadi
Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-
Hivyo
kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika
kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa
na Mungu atakubariki.
Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
No comments:
Post a Comment