Thursday, March 16, 2017

SAFARI YA BAISKELI KUTOKA MBEYA KWENDA KYELA KM 120. Uyole cultural tourism enterprises kwa kushirikiana na Chama cha baiskeli mkoa wa Mbeya na shirika la Elimisha tunawatangazia safari ya baiskeli kutoka mbeya kuelekea Kyela yenye km 120 siku ya 18/03/2017 na 19/03/2017. Lengo la safari hii ni kuutangaza mchezo wa baiskeli na kutangaza utalii katika mkoa wa Mbeya. Katika safari yetu yapo mambo mbalimbali tutajifunza kama mji wa zamani wa Tukuyu, majengo ya kihistoria, maji moto kyela, daraja la kamba,msitu wa katago, maisha na shughuri za watu wa Tukuyu na Kyela na mengine mengi Tutakuwa na team ya watu kumi na moja (11) waendesha baiskeli na gari ya escort mpaka kyela na kisha kufanya camping, na Nyama choma (BBQ). Kama wewe ni mwendesha baiskeli na ungependa kushiriki nafasi bado zipo na ni bure kabisa njoo na baiskeli yako tu, lakini kama wewe si mwendesha baiskeli na ungependa kushiriki kwa lengo la kutalii basi utachangia 20,000/= ikihusisaha usafiri na Malazi. Shukrani za dhati kwa Hollywood restaurant iliyopo kyela ktk jengo la KBC kwa kutuunga mkono, tunakaribisha wadau wengine ili tuweze kuungana pamoja, Kwa mawasiliano zaidi piga simu no 0783545464 au 0766422703

Post a Comment