Saturday, May 6, 2017

AFYA YAKO- Faida za kula Machungwa kiafya katika mwili wako



Machungwa ni miongoni mwa matunda ya msimu, ambapo kwa hapa Tanzania hupatikana kwa wingi katika mkoa wa tanga. Tukiachana na hayo je wewe ni mtumiaji wa machungwa? Kama jibu ni ndio, basi nichukue fursa hii kikupongeza sana.

Na kwa wewe ambaye huna mazoea ya kutumia machungwa ni vyema ukaanza kutumia kuanzia leo kwani watalamu wanasema mtu anapotumia machingwa kuna uwezekano mkubwa kuweza kuzuia magonjwa yafuatayo.

1. Ukosefu wa choo.
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.

2. Shinikizo la damu
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.

3. Ulaji wa chungwa hutibu maginjwa ya moyo.
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!

4. Husaidia katika kuimarisha afya ya ngozi.
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.

5. Huzaidia uzalishaji wa kinga mwilini.
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.
Post a Comment