Wednesday, May 31, 2017

Dk Mwakyembe amlilia aliyechora nembo ya taifa

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya msanii mkongwe katika fani ya uchoraji Mzee Francis Maige Kanyasu (86), aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Habari, imeeleza kuwa Waziri Mwakyembe  amemwelekeza Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Mngereza, kushirikiana kwa karibu na ndugu na jamaa wa marehemu katika mazishi yake.

“Wizara itahakikisha michango ya wasanii wakongwe kama Mzee Kanyasu, inafuatiliwa kwa karibu na kuwekewa kumbukumbu kwa faida ya vizazi vijavyo.” imesema taarifa hiyo
Post a Comment