Wednesday, May 17, 2017

Makamu wa Rais Samia Suluhu Afungua Mkutano wa Polisi Wanawake SADC

 Makamu wa Rais, Samiah Suluhu, akizungumza jambo kwenye mkutano wa polisi wanawake wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini (SADC).

MAKAMU wa Rais, Samiah Suluhu, leo amefungua mkutano wa polisi wanawake wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaolenga kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matatizo mbalimbali na kubadilishana uwezo wa utendaji kazi.

Mkutano huo uliozinduliwa jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Polisi Inspekta Ernest Mangu, ni wa siku tatu ambapo kuanzia kesho utakuwa ukifanyika katika kumbi zilizopo viwanja vya Mlimani City Dar.

Mkutano huo utazungumzia pia namna ya kuimarisha umoja wa SADC na kuendeleza madawati ya kijinsia katika vituo vya polisi kwenye nchi husika.


 Baadhi ya polisi wanawake wa SADC wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano.


Washiriki wa mkutano wakiingia ukumbini.

No comments: