Monday, May 15, 2017

Mbunge wa Kibiti ahofia maisha yake

Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Ally Ungando (CCM), amekataa kuzungumzia matukio ya kihalifu na mauaji yanayotokea katika eneo hilo, kwa kuhofia usalama wa maisha yake.

Hatua hiyo ni baada ya kuuawa kwa aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani Kibiti, Arife Mtulia, Gazeti la MTANZANIA lilimtafuta mbunge huyo ili kupata maoni yake.

“Sina comment yoyote juu ya mauaji hayo kwa sababu hata mimi ni binadamu nahofia usalama wangu pia vilevile,” alisema Ungando.

Kuuawa kwa kada huyo wa CCM ambaye alipigwa risasi na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake, ni mwendelezo wa mauaji ya watu mbalimbali, wakiwamo askari wa Jeshi la Polisi na viongozi wa Serikali za vijiji mkoani Pwani.
Post a Comment