Tuesday, May 16, 2017

Mtoto wa miaka 10 aruhusiwa kutoa mimba India

Jopo la madaktari limekubali ombi la msichana wa umri wa miaka 10, ambaye ni muathiriwa ya ubakaji kutoka jimbo la Haryana kaskazni mwa India la kutoa mimba.

Dr Ashok Chauhan amesema kuwa hatua hiyo sasa inaweza kuchukuliwa wakati wowote.
Msichana huyo alipata ujauzito karibu miezi mitano iliyopita. Anadaiwa kubakwa na baba wa kambo ambaye amekamatwa.

Sheria nchini India haziruhusu utoaji mimba baada ya wiki 20, bila ya idhini ya madaktari kuwa maisha ya mwanamke mjamzito yako hatarini.

Uamuzi wa kumruhusu msichana huyo kutoa mimba ulichukuliwa baada ya mahakama kuwaambia madaktari kuwa itakubali.
India ni nyumbani kwa idadi kubwa ya watoto wanaodhulumiwa kingono.

Hata hivyo hakuna nguvu ya kuzungumzia suala hilo wazi na ni nadra kuzungumziwa hadharani.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kesi nyingi kama hii ya mtoto wa miaka kumi, wale wanaotekeleza ni watu wanaofahamika kwa watoto wenyewe hasusan wanaowatunza kama wazazi, jamaa na walimu.

No comments: