Thursday, May 18, 2017

Mwanafunzi aliyefariki Udom asafirishwa Mbeya kwa maziko.

Dodoma.
 Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) umesema mwanafunzi Sarah Mwansasu amefariki dunia kutokana na maradhi ya kifafa yaliyokuwa yakimsumbua.

Ofisa Habari wa Udom, Beatrice Mtenga amesema Mwansasu aliyekuwa anasoma kozi ya uhandisi akiwa mwaka wa pili alikuwa akitumia dawa za ugonjwa huo.

"Juzi alitoka kujisomea na alipolala alipatwa na kifafa kilichosababisha akorome kwa kuwa alikuwa amelala kifudifudi," amesema Mtenga alipozungumza na gazeti hili.
Mtenga amesema alikuwa akikoroma kwa sauti kubwa ndipo wenzake walipoamka na kumpeleka hospitali ambako waliambiwa alishafariki dunia.

Amesema mwili wa Mwansasu umesafirishwa leo (Alhamisi) kupelekwa kwao Mbeya kwa maziko.

Mwanafunzi wa chuo hicho, Jackson Azimio amesema kabla ya kifo chake, Mwansasu alishiriki mjadala pamoja na wanafunzi wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mtihani ya majaribio.
Post a Comment