Sunday, May 28, 2017

Nahodha wa Simba Jonas Mkude apata ajali mbaya

Baada ya jana kuiongoza timu yake ya Simba SC kurejea katika anga ya kimataifa kwa ushindi wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC, kiungo wa Simba Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali mbaya akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.

Nahodha huyo wa Simba amepata ajali hiyo maeneo ya Mitibora, Dumila mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kuiwahi Taifa Stars. Taarifa za awali zinasema ameumia maeneo ya shingoni, amekimbizwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wenzie ambao baadhi wana halimbaya.

Kwenye gari ambayo Mkude amepata nayo ajali walikuwepo watu 6, na kilichopelekea ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la nyuma. Majeruhi mmoja yuko mahututi.

Tutaendelea kujuzana hali yake na majeruhi wengine kadri taarifa zitakavyokuwa zinatoka.


Post a Comment