Sunday, May 28, 2017

Picha ya Shabiki wa Simba aliyepoteza maisha katika ajali aliyokuwemo Jonas Mkude

Shose Fidelis ndiye aliyepoteza maisha katika ajali ya gari ambalo alikuwamo Nahodha wa Simba, Jonas Mkude.

Mkude ni katika ya majeruhi watatu na Shose ambaye aliambatana na wenzake kwenda kuishangilia Simba ikipambana kuwania Kombe la Shirikisho, amepoteza maisha.

Shose amekuwa katika ya mashabiki wakubwa wa Simba na amekuwa akionekana pamoja katika lile Kundi la Wapenda Soka ambalo linaundwa na mashabiki wa Simba.

Mkude alikuwa njiani kutoka Dodoma kurejea Dar es Salaam baada ya jana Simba kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho.

Mkude alikuwa katika gari na baadhi ya mashabiki wa Simba na gari lilipasuka tairi na kuanguka. Mtu mmoja amefariki dunia.


Post a Comment