Saturday, May 20, 2017

Rais Bashir akataa kuonana na Trump Saudia

Rais wa Sudan Omar el-Bashir ameamua kutoitikia mwaliko kutoka Saudia kuhudhuria mkutano wa mataifa ya Kiislamu ambao rais Donald Trump atakuwa mgeni.

Bwana Bashir ambaye alitoa sababu za kibinafsi anasakwa kwa uhalifu wa kivita katika eneo la Darfur na Marekani ilikuwa haikufurahia mwaliko wake katika mkutano huo.

Sudam ilikuwa imesema kuwa inataka kuimarisha uhusiano wake na Marekani katika mkutano huo.
Saudia ndio taifa la kwanza la ziara ya kigeni ya bwana Trump.

Taarifa ya ya afisi ya rais Bashir ilisema kuwa rais huyo aliomba msamaha kwa mfalme Salma wa Saudia kwa kushindwa kuhudhuria mkutano huo wa Riyadh.

Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa, Waziri wa maswala ya mataifa ya kigeni Taha al-Hussein atamwakilisha.

Mwaka 2002 na 2010, mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC ilitoa agizo la kukamatwa kwa rais Bashir kwa mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita na uhaifu dhidi ya binaadamu katika eneo la Darfur ambapo takriban watu 300,000 waliuawa.

No comments: