Saturday, May 6, 2017

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA VIFO VYA WANAFUNZI KATIKA AJALI KARATU

................................................................................................
Binti (picha no. 1) ni mmoja wa wanafunzi watatu walionusurika akitoka kwenye ajali hiyo bila hata mkwaruzo wa jani au mti. Hapo wazazi wake wakidaiwa kushangaa mara baada ya ajali hiyo. Picha no. 2, binti huyo (pembeni kabisa kulia akiipa mgongo kamera), akiwa na wenzake kabla ya kuanza safari ya kuelekea Karatu. Nb: kama ndivyo mimi sishangai, kwani uwezo wa Mungu naujua, ila kidunia, haya ni maajabu ya 8 ya Dunia... Mungu ashukuriwe kwa kila jambo.
..................................................................................
Watu 36 wamepoteza maisha huku wawili wakijeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha gari namba T 871 BYS Toyota costa lililokuwa linasafirisha wanafunzi wa shule ya Luck vicent waliokuwa wanatokea jijini Arusha kwenda shule ya msingi Tumaini Iliyoko wilayani Karatu kwa ajili ya masomo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo Amesema kuwa wanafunzi 33 wakiwemo walimu 2 pamoja na Dereva aliyekuwa anaendesha gari hilo.

Kamanda MKUMBO amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya SAA tatu asubuhi wakati mvua inanyesha ambapo mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.

Amesema kuwa baada ya ajali hiyo miili yote 36 imepelekwa katika hospital ya Lutheran karatu kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuipeleka Mount Meru Arusha kwa ajili ya ndugu zao kuitambua na taratibu za mazishi ziendelee ambapo uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.

Mkurugenz wa Jiji la ARUSHA Athumani Kihamia amewasihi wazazi pamoja na wana Arusha kuwa wavumilivu kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba mzito uliotokea katika Jiji la Arusha

Naye Mwalimu wa shule ya msingi Luck vicent ambaye ndiye mlezi wa wanafunzi hao Bwana Efrem Jackson amesema kuwa watoto hao walikuwa wanaenda Karatu kwa ajili ya ujirani mwema na shule ya msingi ya Tumaini iliyoko Karatu kwa ajili ya masuala ya kimasomo.

Jumla ya watu waliokuwemo Ndani ya Gari hilo ni 38 waliopoteza maisha ni 36 wawili  ni majeruhi.
............................................................................................
Post a Comment