Monday, May 22, 2017

Serengeti Boys yatupwa nje ya michuano ya AFCON U-17

Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imetolewa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17, baada ya kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, Gabon.

Matokeo hayo yanazifanya Niger na Tanzania kuwa sawa kwa pointi na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo mshindi katika mechi baina yao amefuzu Kombe la Dunia Oktoba mwaka huu India na pia kwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo Niger inaungana na Mali ambayo inaongoza kundi kwa pointi zake saba, baada ya ushindi wa mechi mbili na sare moja, wakati Tanzania na Angola zote zikiaga mashindano hayo.
Kwa ujumla, Serengeti Boys ilizidiwa katika mchezo huo kwa kipindi cha kwanza na cha pili hali iliendelea kuwa hivyo na hatimaye Niger wakatoka kifua mbele kwa kuitoa Tanzania.

No comments: