Saturday, May 20, 2017

Sumaye ajiuzulu ujumbe wa bodi CRDB

Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Mashariki, Frederick Sumaye, amejiuzulu ujumbe wa bodi ya Benki ya CRDB ili atekeleze zaidi majukumu yake ya kisiasa.

"Nina shughuli nyingi za kisiasa ambazo zitaninyima nafasi ya kuhudhuria vikao vya bodi.  Sipendi pia kuona CRDB ikihusishwa na msimamo wangu kisiasa. Hii ni taasisi huru ambayo ina wanahisa wengi ambao sitapenda kuona maslahi yao yakiingiliwa kutokana na siasa,"  amesema Sumaye.
Post a Comment