Wednesday, June 14, 2017

Barrick yafanya mazungumzo na Rais JPM na kuahidi Tanzania kulipa na kujenga Mtambo wa Kuchenjua dhahabu

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold ya Canada, Profesa John Thornton amesema atashirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu hapa nchini (smelter).

Profesa Thornton ameyasema hayo leo (Jumatano) Ikulu  alipokutana na Rais John Magufuli kwa ajili ya kujadiliana kuhusu sakata la mchanga wa madini.

Pia, Profesa Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

No comments: