Tuesday, June 13, 2017

Je Saif al-Islam Gaddafi anaweza kuiongoza Libya?

Saif al-Islam Gaddafi

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGaddafi alikamatwa na kikosi cha wanamgambo mwaka wa 2011 na kupelekwa Zintan

Saif al-Islam Gaddafi anasemekana kuwachiliwa huru kutoka jela nchini Libya baada ya miaka sita. Basi ni nini kitakachofuata kwa mtoto huyu wa Kanali Muammar Gaddafi, ambaye wakati mmoja alionekana kuweza kuchukua usukani kutoka kwa baba yake kama kiongozi wa nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika?

Je Saif al-Islam Gaddafi kweli yuko huru?

Kwa mujibu wa kikosi cha wanamgambo kilichokuwa kimemshika na kumzuia tangu mwaka wa 2011, pamoja na mmoja wa mawakili wake, ni kweli yuko huru. Hata hivyo, pande zote mbili zilidai vivyo hivyo Julai mwaka jana. Mwishowe, ilipatikana si kweli - angalau si katika maana ya kawaida inayoeleweka ya kuwa huru.
Anaweza kuwa hakutazamwa kama "mtu huru", katika nadharia, katika mwaka uliopita na kikosi kilichomzuia. Lakini hakukuwa na ushahidi wakati huo, wala yeyote kwa sasa, kwamba amewahi kutoka nje ya Zintan, ambako amezuiliwa

Mbona kutangazwa kuachiliwa kwake wakati huu?

Ni vigumu kuielewa Libya na siasa yake ya uanamgambo. Hakuna mtu anayeweza kusema hakika ni kwa nini kuachiliwa kwake kumetangazwa wakati huu lakini baadhi wanaamini inaweza kuhusika na mgogoro unaoendelea kati ya makundi pinzani ya wanamgambo na makundi ya kisiasa.

Yuko wapi?

Hatujui. Hadi sasa wakili wake hajafichua aliko mteja wake kwa "sababu za kiusalama".
Kama ameondoka Zintan, inaaminiwa alikwenda mashariki mwa Libya.
Wengine wanaamini alikwenda kusini, na baadhi wanafikiri kuna uwezekano mkubwa wa Gaddafi kuelekea katika mji wa Bani Walid zaidi ya mahali penginepopote. Hii ilikuwa ni moja ya maeneo ya mwisho kuanguka wakati wa vita vya 2011 ambavyo vilimwondoa baba yake mamlakani na bado inazingatiwa na Walibya makazi ya wafuasi wa serikali ya zamani.
Wengine wamependekeza kuwa anaweza kuwa Misri.

Saif al-Islam GaddafiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSaif al-Islam Gaddafi alikuwa mfuasi shadidi wa baba yake, na aliwatishia wapinzani, huku waasi wakiivamia Libya mwaka 2011

Je, mpango wake ni upi?

Hii itakuwa bayana ikiwa atatoa taarifa. Wakili wake amedai kuwa Gaddafi anaweza mtu wa kutegemea katika juhudi za kuleta maridhiano ya kitaifa.

Je, anaweze kuingia tena katika siasa?

Nchini Libya kila kitu kinawezekana. Tangu 2011, wanachama na taasisi za serikali ya kale yamerejea mamlakani, angalau katika uwezo tofauti. Hata hivyo, kama Gaddafi atajaribu hii, ataabiliana na vituo vingi ya madaraka.

Je, anaweza kusafiri ndani ya Libya?

Kinadharia, ndiyo, lakini si kwa uhuru au kwa urahisi. Baadhi ya vikosi vilivyo na nguvu zaidi nchini vitakasirishwa na ripoti za kuachiliwa kwake na kuna uwezekano wa kujaribu kumkamata tena.

Ni nini kinachotokea kwa hukumu ya kifo dhidi yake?

Mahakama ya Tripoli iliyomhukumu haijaifutilia mbali na haionekani kana kwamba kuna mpango wowote wa kufanya hivyo.
Mwendeshaji mkuu wa mashtaka, aliye Tripoli, pia haamini sheria ya msamaha, iliyopitishwa na bunge mjini, inafaa kutumika kwa Gaddafi.
Wanamgambo waliomwachilia walitaja sheria hii wakitangaza kuachiliwa kwake - na walidai kuwa walikuwa wanafuata taratibu za kisheria.

Saif al-Islam Gaddafi: Mrithi wa mfungwa

Juni 1972: Alizaliwa Tripoli, Libya, mwana wa pili wa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi
Februari 2011: Upinzani dhidi ya serikali ya Gaddafi inaanza
Juni 2011: Mahakama ya Kimataifa yatoa kibali cha kukamatwa kwake kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu
Agosti 2011: Anaondoka mji mkuu baada ya Tripoli kudhibitiwa na vikosi vilivyopinga serikali; akakimbilia Bani Walid
Oktoba 2011: Baba na ndugu mdogo wauawa
Novemba 19, 2011: Alitekwa na wanamgambo alipokuwa akijaribu kukimbilia kusini mwa Niger. Akafungwa Zintan
Julai 2015: Alihukumiwa kifo na mahakama ya Tripoli
Juni 2017: Inasemekana aliachiliwa chini ya sheria ya msamaha iliyotolewa na mojawapo ya serikali mbili za mashindano nchini Libya

Saif al-Islam GaddafiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionGaddafi alifika mbele ya mahakama ya Zintan mwaka wa 2014

Je, Walibya wanafikiria nini kuhusu Gaddafi sasa?

Kwa baadhi, yeye daima atakuwa mwana wa dikteta wa zamani ambaye alimuunga mkono sana baba yake hadi kufariki kwake, na ambaye anadaiwa kuchangia pakubwa katika kuagiza mauaji ya waandamanaji.
Kwa wengine, ambao wakati mmoja wamwona kama mrekebishaji ndani ya serikali ya baba yake, yeye anaweza kuwa mtu nguvu ya kutosha kukomesha machafuko nchini.

Nani wanatarajiwa kumuunga mkono au kumpinga ndani ya Libya?

Kuna orodha ndefu ya wanamgambo, wanasiasa, wafanyabiashara mashuhuri na Walibya wa kawaida ambao watampinga.
Lakini baadhi ya Walibya ambao wameteseka tangu baba yake atolewe mamlakani 2011 wanaweza kumuunga mkono.
Saif al-Islam Gaddafi pia anaweza kuungwa mkono na baadhi ya vikosi vya jeshi na vya kisiasa, wakiongozwa na mwanajeshi, Khalifa Hefter.

Tunajua nini kuhusu ya maoni yake ya kisiasa juu ya Libya leo hii?

Hakuna tulichosikia kutoka kwake moja kwa moja, tangu kuzuiliwa kwake.
Lakini tukizingatia wanachosema mawakili wake - wa zamani na wa sasa - anaonekana kufikiri nchi imegawanyika na anweza kusaidia kutatua hilo.

Je, anaweza kusafiri nje ya Libya?

Anaweza.
Hata hivyo, bado anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ya Hague, ambayo inataka kumfungulia mashtaka kuhusiana na uhalifu wa kivita uliofanywa wakati wa mchafuko wa 2011.
Kwa nadharia, kama atasafiri kuelekea nchi yoyote ambayo imeridhia ICC, nchi hiyo itakuwa na wajibu wa kumkamata na kumkabidhi kwa Hague.

Nchi zingine duniani zitasema nini ikiwa atarudi madarakani?

Nchi nyingi duniani zilionekana kuchangia kumtoa baba yake madarakani, na ni wazi kuwa Marekani, uingereza na Ubelgiji havitafurahia.
Hata hivyo, kuna imani kati ya Walibya kwamba serikali za Magharibi ziko tayari kufanya kazi na mtu yeyote ambaye angeweza kuleta udhibiti na utulivu nchini, bora tu awe na maoni yanayoambatana na shera zao..

Je Walibya wengi wanatamani siku nzuri za zamani za Kanali Gaddafi?

Leo hii, ndiyo wanatamani.
Uongozi wa Gaddafi bado unahusishwa sana na udhalimu na ni wakati ambao Walibya wengi hawapendi kukumbuka - lakini wengi pia wanahisi kwa sasa uongozi huo ni afadhali na ni "uovu mdogo" kulingana na hali ilivyo sasa.
Raia wanatamanini utulivu na wakati ambao maisha yao tena hayatazongwa na na migogoro ambayo ina tikisatikisa nchi.

No comments: