Tuesday, June 13, 2017

Serikali yajipanga kuandaa rejista ya watu wenye ulemavu kuanzia ngazi za vitongoji.

Serikali imesema iko kwenye mkakati wa kuandaa rejista ya watu wenye ulemavu kuanzia ngazi za vitongoji vijiji kata na halmashauri ili kuwa na rekodi inayoonyesha  idadi yao ambayo pamoja na mambo mengine hali itasaidia kupatiwa huduma muhimu wanazostahili ikiwemo ulinzi.

Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelewa juu ya Ualbino Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera, bunge, kazi ,ajira na walemavu Mhe Jenista Muhagama anasema kuwepo kwa rejista hiyo kutasaidia serikali kutambua idadi ya watu wenye mahitaji maalum na kuwafikishia huduma wanazostahili wa urahisi ikiwemo ulinzi kwa watu wenye ualbino

Akizungumzia siku hiyo Mjumbe wa Bodi ya Chama cha wenye ualbino Sizya Migila anasema bado kuna changamoto mbalimbali zinazolikabili kundi hilo ikiwemo unyanyapaa huku wakiiomba serikali kuweka fungu maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na sheria Bwana Amon Mpanju anapongeza jitihada za Rais John Pombe Magufuli la kuwakumbuka kwa kuwapatia nafasi watu wenye ulemavu huku baadhi ya watu wenye ualabino wakizungumzia umuhimu wa siku hiyo kwao
.

No comments: