Monday, June 12, 2017

Tanzania yapoteza matrilioni ya pesa kupitia usafirishaji mchanga wa madini

Rais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini

Haki miliki ya pichaIKULU DAR ES SALAAM
Image captionRais Magufuli akihesabu makontena yenye mchanga wenye madini
Tanzania imepoteza takriban shilingi za kitanzania trilioni 188 (dola bilioni 84 za Marekani ) katika kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba.
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi March mwaka huu na Rais Dr John Pombe Magufuli.
Ripoti hii imekuja siku chache baada ya Ripoti ya kwanza iliyojikita kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na usafirishaji wa mchanga wenye madini.
Kamati hii ya sasa iliundwa na wataalam wa masuala ya uchumi na wanasheria ambao walikuwa na jukumu la kutazama mikataba ya madini na athari za kiuchumi kwa Tanzania.
Katika Ripoti ya Jumatatu, Tume imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi yake nchini Canada, Acacia ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi kusajiliwa nchini humo, hivyo imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.
Rais Magufuli akiangalia jinsi magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halaliHaki miliki ya pichaIKULU DAR ES SALAAM
Image captionRais Magufuli akiangalia jinsi magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halali
Katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni kutoka Ikulu, Rais Magufuli amemtaka waziri wa sheria Profesa Paramagamba Kabudi kupitia mikataba yote ya madini.
Ameahidi kutekeleza mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati.
Ripoti iliopita ilisababisha Waziri wa nishati na madini Prof Sospeter Muhongo kusimamishwa kazi.

No comments: