Wednesday, June 14, 2017

Watu kadha wafariki baada ya moto kuteketeza jengo refu London

Grenfell Tower Fire

Image captionIdara ya wazima moto jijini London imetuma malori 40 ya kuzima moto huo
Watu kadha wamefariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London.
Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, ambapo walioshudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada.
Zaidi ya watu 50 wanatibiwa hospitalini.
Mwandishi wa BBC alisema kuwa kulikuwa na hofu kuwa jengo hilo lingeporomoka.
Moshi unaweza kuonekana kutoka mbaliHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMoshi unaweza kuonekana kutoka mbali
Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza mwendo wa saa 01:16, saa za Uingereza.
Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo.
Sehemu kubwa ya jengo ilishika motoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSehemu kubwa ya jengo ilishika moto
 jengo hilo liikubwa na kuna na wasiwasi wa kuanguka.
Grenfell Tower Fire
Image captiontakribani wazima moto 200 wanapambana nao.

No comments: