Monday, July 3, 2017

Alvaro Morata akaribia kutua Man United

UHAMISHO wa Alvaro Morata kwenda Manchester United unakaribia kukamilika baada ya wakala na baba wa mshambuliaji huyo kuhudhuria kikao cha mazungumzo na Real Madrid Jumatatu.

Taarifa nchini Hispania zimesema kwamba Juanma Lopez na Alfonso Morata walikwenda katika ofisi za Real mida ya mchana kukutana na viongozi.

Kikao hicho kilimalizika baada ya muda wa saa moja kwa mujibu wa AS na thamani ya Morata ambaye anatakiwa sana na Manchester United ni Pauni Milioni 70.

Pamoja na hayo, Mashetani hao Wekundu bado hawajaafiki bei ya manunuzi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye amefunga mabao 20 katuika mechi 43 msimu uliopita.

Taarifa za kikao baina ya Lopez na Real azinazidi kuongeza uwezekano wa uhamisho huo.
Post a Comment