Wednesday, July 26, 2017

Makontena 10 ya kemikali yakamatwa Bandarini, Dsm

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imekamata makontena 10 yenye lita 200,000 za kemikali bashrifu katika Bandari ya Dar es Salaam yenye ambayo yameingizwa kutoka nchini Swaziland kinyume cha sheria.

Aidha mamlaka hiyo imebaini kuwa, kampuni inayotuhumiwa kwa sakata hilo imekuwa ikiingiza kemikali hizo tangu mwaka 2016, ambapo taarifa zinaonyesha waliwahi kuingiza lita milioni 1.5 za kemikali bashirifu ambazo zinaonyesha zilipelekwa kwenye kampuni moja iliyoko Mbezi Luis.

Baada ya kufuatilia wakagundua kuwa kampuni hiyo inajihusisha na yard ya magari na siyo kutunza wala kuchakata kemikali jambao ambalo liliwapa wasiwasi na kuamua kufanya uchunguzi zaidi.

No comments: