Wednesday, July 12, 2017

Wachezaji wa Everton watua Dar es Salaam Tanzania tayari kukabili Gor Mahia

Rooney na wachezaji wa Everton

Wachezaji wa klabu ya Everton kutoka England wamewasili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ziara yao ya kwanza kabisa Afrika Mashariki.
Wachezaji hao na wakufunzi pamoja na maafisa wengine wa timu walifika uwanja wa ndege saa mbili asubuhi kutoka Liverpool.
Ziara yao ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi ya Premia.
Miongoni mwa wachezaji waliosafiri Tanzania ni Wayne Rooney ambaye amerejea katika klabu hiyo bila kulipiwa ada yoyote baada ya kukaa miaka 13 klabu ya Manchester United.
Wachezaji wa Everton
Mashabiki wengi wa soka ya England wamesafiri Tanzania kushuhudia Everton wakichuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika uwanja wa taifa wa michezo jijini Dar es Salaam.
Uwanja huo una uwezo wa kutoshea mashabiki 60,000.
Rooney anatarajiwa kucheza katika mechi hiyo ya Alhamisi.
Wengi wa mashabiki waliofika nje ya hoteli wanamokaa Everton jijini Dar es Salaam waliimba "Rooney Rooney" mchezaji huyo aliposhuka kutoka kwenye basi kuingia hotelini.
Kulikuwa pia na kundi la raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao walijawa na furaha kumuona mwenzao Yannick Bolasie.
Wachezaji wa Everton
Wachezaji ngoma wa Kimaasai waliofika kuwatumbuiza wachezaji hao
Image captionWachezaji ngoma wa Kimaasai waliofika kuwatumbuiza wachezaji hao
Wachezaji wa Everton
Waliimba nyimbo za kitamaduni za DR Congo naye Bolasie akawajibu kwa kucheza.
Mechi ya kesho imeandaliwa na kampuni ya SportPesa kusherehekea udhamini wa jezi za klabu ya Everton.
Wakati wa ziara yao, wachezaji wa Everton pia wataandaa vikao vya mafunzo ya soka na kucheza pia dhidi ya timu mseto ya wachezaji wenye matatizo ya ngozi, Albino United, kuhamasisha watu kuhusu mashambulio na dhuluma ambazo zimekuwa zikitendewa watu wenye ulemavu huo.
Wengi wamekuwa wakiuawa Tanzania na nchi jirani kwa sababu ya ushirikina.
Wachezaji hao baadaye wameelekea shule ya watoto wenye ulemavu ya Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.
Shule hiyo hupokea ufadhili kutoka kwa shirika la kutoa msaada nchi za nje la Uingereza, DFID.
Baadaye, wachezaji hao wanatarajiwa kucheza na watoto hao.
Wachezaji wa Everton wakiwa shule ya Uhuru Mchanganyiko
Image captionWachezaji wa Everton wakiwa shule ya Uhuru Mchanganyiko
Wachezaji wa Everton wakiwasalimia watoto
Image captionWachezaji wa Everton wakiwasalimia watoto
Kuwasalimia watoto
Mchezaji wa Everton akiwa amejifumba macho tayari kucheza na watoto
Image captionMchezaji wa Everton akiwa amejifumba macho tayari kucheza na watoto

No comments: