Wednesday, August 16, 2017

Mamia ya watu wazikwa, Sierra Leone

Maeneo ya milimani ndio yaliyoathirika zaidiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaeneo ya milimani ndio yaliyoathirika zaidi
Wiizara ya afya nchini Sierra Leone imesema takriban nusu ya maiti 400 zitokanazo na maporomoko ya udongo na mafuriko nje ya mji wa Freetown tayari zimezikwa.
Serikali ilisema mazishi ya pamoja yangeahirishwa hadi leo ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kutambua miili ya maiti ya waathirika.
Lakini mkuu wa wataalamu wa magonjwa kutoka mjini Freetown ameiambia BBC kwamba baadhi ya mazishi yalikuwa yamefanyika.
Imefahamika kuwa mazishi hayo yamehusisha miili ambayo tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika kabisa.
Watu wapatao mia sita mpaka sasa bado hawajulikani walipo.
Rais wa Sierra Leone ametangaza siku saba za maombolezi.
Nathaniel Williams ni daktari katika hospitali kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.
Ameongeza kusema kuwa hivi sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea.

No comments: