Thursday, February 22, 2018

Rais wa FIFA: Tanzania ni nchi ya soka

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni InfantinoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino
Rais wa Shirikisho la Soka la duniani (FIFA) Gianni Infantino, akiwa nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa shirikisho hilo nchini.
Mkutano huo ulishirikisha jumla ya mashirikisho 21 ya kandanda ambao ni wanachama wa shirikisho hilo.
Rais wa shirikisho hilo la soka duniani alikutana na Waziri Mkuu wa nchi , Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Utamaduni na Michezo Harryson Mwakyembe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Infantino amesisitiza kuzungumzia hali ya rushwa katika mpira wa miguu.
"Tumefanikiwa sana katika kuweka uwazi wa matumizi ya fedha za FIFA. Leo FIFA ni shirikisho lenye uwazi. Tunachapisha matumizi ya fedha zote. Kila mtu anaweza kufuatilia fedha zinatoka wapi na fedha zinaenda wapi."
Akizungumzia jitihada za kukuza soka barani Afrika, Bw Infantino ameelezea kuwa siku za nyuma Afrika ilikuwa inapata dola za kimarekani milioni 26 kutoka FIFA, lakini sasa hivi, Afrika inapata dola za kimarekani milioni 100 ili kuiinua mchezo wa soka.
Pamoja na hayo amesema katika kipindi chake amejaribu kuhakikisha ongezeko la timu za Afrika katika kushiriki michuano ya kombe la dunia .
Tangu aingie madarakani ,Rais huyo wa Fifa ameongeza idadi ya timu zitazoshiriki michuano ya kombe la dunia la mwaka 2026 toka 5 mpaka 7.
"Sitaki kuahidi lolote, ninatenda" Infantino ameelezea.
Mchezo wa kandanda ya wanaume unafuatiliwa sana na una uwekezaji mkubwa duniani, matokeo ni kwamba mchezo huo kwa upande wa wanawake unaachwa nyuma.
Ajenda kubwa katika mkutano huo ilikuwa kujadili namna ya kukuza soka la wanawake na vijana pamoja na suala la usajili kwa njia ya mtandao.
Gianni amesema wamezungumzia kuanzisha ligi ya kimataifa ya wanawake.
"Tunataka kuzindua michuano mpya ya FIFA, ligi ya kimataifa ya wanawake. Tutaomba nchi zote kushiriki na tutatoa msaada wa fedha "
Mkutano wa Fifa una kauli mbiu ya "kurejesha kandanda kwa Fifa na Fifa kwa kandanda.

No comments: