Thursday, February 2, 2023
Monday, December 19, 2022
Dkt. Mpango kuzindua kongamano la Wahariri na wadau wa mazingira
Leo Disemba 19, 2022 Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasili kwenye kongamano la wahariri na Wadau wa uhifadhi mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji Mkoani Iringa lilioandaliwa na Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA)
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na HabibMchange Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Raslimali na Taarifa (MECIRA) mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la wahariri na Wadau wa uhifadhi mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji Mkoani IringaMakamu wa Rais Dk.Philip Mpango akikagua mabanda katika viwanja vya ukumbi wa Masiti mjini Iringa alipowasili kuhudhuria Kongamano la Wahariri na wadau wa uhifadhi wa Mazingira na Utunzaji Vyanzo Vya Maji lilioandaliwa na MECIRA.Baadhi ya viongozi na wadau wa uhifadhi mazingira na utunzaji vyanzo vya maji wakifuatilia kwa makini kinachoendelea katika kongamano la wanahabari na wadau wa uhifadhi mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji linaoendelea katika ukumbi wa Masiti mjini Iringa
Sunday, December 18, 2022
Serikali yamega eneo la ranchi na kuwapa wananchi
Kauli hiyo imetolewa leo na Kamati ya Mawaziri wa Kisekta katika mkutano wa hadhara mazingira katika eneo la Shule ya Msingi Rutoro, Muleba .
Mkutano mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, amesema hayo maeneo yatamegwa na kutoa wananchi kwa ushauri wa ushauri wa watalaam.
"Maeneo yatakayomegwa kwa ushauri wa kufanya maamuzi kuhusu biashara yatawekewa utaratibu wa kutuma na uongozi wa mkoa ukishirikiana na wilaya ili msigombanie kufanya jambo lolote katika maeneo hayo," Amesema Waziri Ndaki
Katika hatua nyingine, amesema serikali imeridhia kukiacha Kitongoji cha Rwamisha B ambacho kiko wilaya ya Karagwe chenye kaya 480 ambacho awali kiliamuliwa kiondoke.
Sambamba na hilo Waziri Ndaki amewatoa hofu walioko katika ranchi ya Kagoma akiwaeleza kuwa wako salama na serikali imefanya mazungumzo na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ili uwekwe utaratibu mzuri ambao utawawezesha maeneo yatakayomegwa.
Naye, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhi Kikwete, amewataka wananchi kuheshimu sheria za ardhi hususani katika mpango wa maendeleo ya ardhi na kwamba kuna kazi ya kufanya katika ujenzi wa majengo ya majengo ya eneo la Rutoro yanakaa sawa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewataka wananchi wa Kata ya Rutoro kutumia ardhi waliyoyachiwa kwa maendeleo kwa miradi ya upandaji miti pamoja na ufugaji nyuki.
Ametoa wito kwa wananchi kutoyavamia maeneo yatakayoachwa kwa serikali kwa kuwa maeneo yanayotunzwa kwa faida ya kizazi cha leo na kinachokuja.
Kamati ya Mawaziri ya Kisekta imehitimisha ziara yake mkoani Kagera na itaendelea na zoezi hilo katika mkoa wa Ruvuma.
KINGOTANZANIA
0752 881456
Saturday, December 17, 2022
Punguzeni viboko na vitisho kwa wanafunzi - Dkt. Mtahabwa
![]() |
Naye Mwenyekiti wa Wakuu wa vyuo vya Serikali, Tanzania Bara Agustine Sahili amesema wamenufaika na mradi huo kwa kupata mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo vyote.
WHO yasema mabadiliko ya hali ya hewa yahusika na ongezeko la milipuko ya kipindupindu duniani mwaka 2022
Shirika la Afya Duniani linasema mabadiliko ya hali ya hewa yanahusika na ongezeko la idadi ya kesi za milipuko ya kipindupindu kote duniani mwaka 2022.
Takriban nchi 30 zimeripoti milipuko ya ugonjwa huu unaoweza kusababisha vifo ambao umetokea mwaka huu, ambapo kuna ongezeko la juu zaidi kuliko ilivyo kawaida.
Phillippe Barboza ni kiongozi wa timu ya WHO kwa kipindupindu na magonjwa ya kuharisha. Anasema milipuko mikubwa sana ya kipindupindu imetokea sambamba na matukio mabaya ya hali ya hewa na yameonekana kuhusishwa moja kwa moja.
“Ukame mbaya sana kama vile, huko katika Pembe ya Afrika, huko Sahel lakini pia katika sehemu nyingine za dunia. Mafuriko makubwa, misimu ya mvua isiyo ya kawaida, vimbunga. Kwa hiyo, kwa mara nyingine tena, milipuko yote hii inaonekana kuchochewa na matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa,” anasema Barboza.
Hakuna ahueni ya haraka inayoonekana. Shirika la Hali ya Hewa Duniani linabashiri kuwa La Nina ambayo ni matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa itadumu hadi mwisho wa mwaka huu. Mwenendo, ambao ni kutoa ubaridi chini ya maji ya bahari, ulitarajiwa kuendelea mpaka mwaka 2023. Hiyo itapelekea vipindi virefu vya ukame na mafuriko na kuongezeka kwa vimbunga.
Hatimaye, maafisa wa afya wanaonya kuwa milipuko ya kipindupindu huenda ikaendelea na kusambaa kwenye maeneo makubwa katika kipindi cha miezi sita ijayo. Barboza anasema kuzuia milipuko ya magonjwa itakuwa ni changamoto.
Anasema uhaba wa chanjo ulimwenguni umeilazimisha WHO kusitisha kwa muda mkakati wake wa utoaji dozi mbili na kugeukia kwenye utoaji wa dozi moja. Hii itawaruhusu watu wengi zaidi kupatiwa chanjo dhidi ya kipindupindu. Hata hivyo, anasema inapunguza kipindi cha kinga ya mwili dhidi ya maambukizi.
Barboza anasema, “kwa hiyo hali itaendelea kuwepo kwa miezi kadhaa ijayo. Hakuna njia muafaka, hakuna suluhisho la ajabu na watengenezaji wanatengeneza idadi kubwa …kwa hiyo, hakuna matumaini kwamba hali itaboreka katika wiki au miezi ijayo.”
Barboza anasema ukosefu wa data unaifanya iwe vigumu kuangalia kwa usahihi idadi ya kesi za kipindupindu ulimwenguni pamoja na vifo. Hata hivyo, anaelezea habari kutoka walau nchi 14 ambazo zinaashiria kuwa kiwango cha wastani cha vifo ni juu ya asilimia moja. Ameongezea kuwa kiwango cha vifo vitokanavyo na kipindupindu ni vibaya huko Haiti ambayo ni kiasi cha asilimia mbili.
Kipindupindu ni ugonjwa mbaya wa kuharisha unaosababishwa na kula chakula kisicho salama au kunywa maji yasiyo masafi. Matibabu yake yanajumuisha kunywa maji mengi. Watu ambao ni wagonjwa sana wanahitaji kuwekea maji mwilini na kula dawa za antibiotiki. Kipindupindu kinaweza kuua ndani ya saa kadhaa kama hakikutibiwa.
KINGOTANZANIA
0752881456
Wadau 1,000 wakutana kujadili sekta ya habari nchini
