ODM Kenya Yamkingia Kifua Magufuli
CHAMA cha Orange Democratic Movement (ODM) cha Kenya,
kimezungumzia uamuzi wake wa kumwalika Waziri wa Ujenzi, Dk John
Magufuli kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni nchini humo, uliozua
mjadala mkubwa nchini.
Desemba 7 mwaka huu, chama hicho cha upinzani nchini Kenya kilimwalika Dk Magufuli kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja vya Kasarani ambako pamoja na mambo mengine, alimpigia debe Raila Odinga ili achaguliwe kuwa Rais wa Kenya katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani.
Hatua hiyo ya Dk Magufuli ilizua mjadala mkubwa, huku Chadema kikidai kuwa ni makosa kwa nchi moja kuingilia siasa za nchi nyingine na kumtaka waziri huyo aeleze kama alitumwa na Serikali au la.
Chadema pia kilimtaka Rais Jakaya Kikwete atolee kauli hatua hiyo ya waziri wake, vinginevyo nchi itakuwa na uhusiano mbaya na Kenya, endapo Raila hatachaguliwa kuwa Rais. Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa ODM, Profesa Peter Anyang’Nyong’ alisema hakuna haja ya Watanzania kumzonga Waziri Magufuli, kwani ujio wake Kenya, ulitokana na mwaliko wa Odinga.
Profesa Anyang’Nyong’ ambaye chama chake cha ODM kilitangaza kuungana na chama kingine cha Wiper Democratic cha Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka katika uchaguzi huo alisema Odinga alimwalika Magufuli kama rafiki yake wa muda mrefu na rafiki wa ODM.
“Waziri Mkuu wetu Odinga ndiye aliyemwalika Magufuli na alimwalika kama rafiki yake wa karibu. Kuja kwake huku (Kenya) kulikuwa safari binafsi. Hakukuwa (kuja) na uhusiano wowote na wadhifa alio nao Tanzania,” alisema Profesa Onyang’Nyong’.
Alisema ziara ya Magufuli iliratibiwa na Odinga ambaye aligharimia kila kitu na kwamba mwaliko huo ulifanywa kwa kuzingatia ushirikiano wa muda mrefu baina yao.
Profesa Anyang’Nyong’ alisema ODM kumwalika Dk Mafuguli ni mwendelezo wa uhusiano wa wanasiasa wa Tanzania na Kenya uliokuwapo tangu enzi za viongozi; Jomo Kenyatta, Tom Mboya na Mwalimu Julius Nyerere ambao walifanya pamoja kazi ya kudai uhuru.
“Kizazi cha sasa lazima kitambue ushujaa wa viongozi wetu wa zamani ambao walituonyesha namna wanavyoweza kufanya siasa kwa pamoja na kufanikisha malengo yao,” alisema na kuongeza:
“Mambo kama haya lazima tuyatambue kwani sisi sote ni wamoja tena tuna shabaha ya kuwatumikia wananchi wetu. Tunapopata viongozi wenye mitazamo inayofanana kama ile ya waasisi wa mataifa yetu lazima tuwaunge mkono na kuwapa fursa.
“Kwetu sisi Magufuli tunamwona kama shujaa tena mtu ambaye anaweza kutoa idea (mawazo) yanayoweza kukusaidia kusonga mbele kwenye siasa.”Alisema Dk Magufuli ana uzoefu mkubwa na mambo ya siasa na ODM wanatambua umuhimu wake katika siasa zao.
Alipuuza madai kwamba kumwalika Dk Magufuli ni kuingilia siasa za Kenya na huenda hatua hiyo ikadhoofisha uhusiano wa kidiplomasia… “ Kuja kwake hakumaanishi kwamba ameingilia mambo ya Kenya au siasa za taifa hili…. Huyu ni rafiki yetu na alikuwa kama mtu wetu wa karibu.”
JK. Akabidhi Nyumba Mpya 35 Za Waathirika Wa Mabomu Ya Ngongo La Mboto
Bila
kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiakata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali
imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole,
Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012
Bila
kujali mvua kubwa inayonyesha, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua
kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba mpya 35 ambazo serikali
imewajengea waathirika wa mabomu Gongo la Mboto katika eneo la Msogole,
Toangoma, Wilaya ya Ilala leo Desemba 13, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa walionufaika na hatua ya
serikali ya kujenga nyumba mpya 35 kwa ajili ya waathirika wa mabomu
Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala jana
Desemba 13, 2012. Mama huyu ambaye alipoteza mume, amejengewa nyumba ya
vyumba vitano pamoja na fremu ya duka
Baadhi
ya nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu
Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama
zinavyoonekana leo Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete
Baadhi
ya nyumba mpya 35 ambazo serikali imewajengea waathirika wa mabomu
Gongo la Mboto katika eneo la Msogole, Toangoma, Wilaya ya Ilala kama
zinavyoonekqana Desemba 13, 2012 baada ya kuzinduliwa na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete
JK Azindua Mradi Wa Kibada
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi mradi wa
ujenzi wa nyumba 290 za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC)
maeneo ya Kibada, Kigamboni, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam
leo December 13, 2012 . Kushoto ni Mama Salma Kikwete, kulia ni Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye, anayefuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mhandisi Kesogukewele Msita , Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Mchechu,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea moja ya
nyumba baada ya kuzindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba 290 za gharama
nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
maeneo ya
Kibada, Kigamboni, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam leo December
13, 2012 . Wa tatu kulia ni Mama Salma Kikwete, kulia ni wa pili
kushoto ni Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mhandisi Kesogukewele Msita , Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Mchechu,
maeneo ya Kibada, Kigamboni, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam leo December 13, 2012, akiwa pamoja na Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye, Naibu Waziri wa Fedha Sara Salum, Mwanaseheraia Mkuu wa Serikali Bw Jaji Frederick Werema, Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile ,Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Mhandisi Kesogukewele Msita , Mkurugenzi Mkuu Bw. Nehemia Mchechu,
PICHA NA IKULU
KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MBARAK ABDULWAKIL AFUNGA MAFUNZO YA AWALI CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA MKOANI MBEYA
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akikagua
gwaride la wahitimu wa mafunzo ya awali kozi namba 26 wa Chuo Cha
Magereza Kiwira mkoani Mbeya.
Gwaride la wahitimu likipita mbele ya jukwaa kwa heshima.
Wahitimu
wa mafunzo ya awali ya kozi namba 26 wa Chuo cha Magereza, Kiwira
mkoani Mbeya wakionyesha uwezo wao wa kujihami wanapopambana na adui.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akimkabidhi
Jesca Simatya zawadi ya heshima kwa kuwa mwanafunzi bora kwa usafi
chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment