Waziri Mwakyembe alisema hayo hii Jumatano alipofanya ziara ya ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ili kujionea namna mamlaka mbalimbali za uwanja zinavyofanya kazi za kupitisha abiria na mizigo.
Dkt.Mwakyembe amesisitiza kwamba suala la madwa ya kulevya limechafua jina la Tanzania kimataifa kwani watanzania wengi wamekuwa wakishikiliwa katika mataifa mbalimbali kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya .
Julai 5 mwaka huu watanzania wawili Agness Gerald na mwenzake Melisa Edward walikamatwa na kuhusishwa na kusafirisha dawa za kulevya za uzito wa kilo 150 zilizokuwa katika mabegi 6 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Or Thambo Afrika Kusini mabegi ambayo yalipita siku hiyo majira ya alfajiri katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere bila ya kukamatwa.
Dkt. Mwakyembe amesisitiza kwamba suala la madawa ya kulevya limechafua jina la Tanzania kimataifa kwani watanzania wengi wamekuwa wakishikiliwa katika mataifa mbalimbali kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya.
...............................................................
BAKWATA YATAKA TUKIO LA KYELA LIFANYIWE UCHUNGUZI
NA JENNIFER CHAMILA – MAELEZO
BARAZA
Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) limeviomba vyombo vya dola kuendelea
kufanya uchunguzi kuhusu tukio la kuvamiwa,kupigwa na kujeruhiwa kwa
Imamu na waumini wa Kiislamu wakiwa msikitini wakati wa swala ya
Idd-el-Fitri iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani
Mbeya na kuhakikisha
hdg
Aidha
baraza hilo limesikitishwa na kitendo hicho, na kuvitaka vyombo hivyo
kuhakikisha kwamba wahalifu wote wanafikishwa mbele ya sheria.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa kwa vyombo vya habari na Mufti wa
Tanzania Sheikh Issa Simba,imelaani kitendo hicho na kusema watu
waliofanya kitendo hicho wamegeuka maagizo ya ya Qur'an Tukufu pamoja na
Sheria za Nchi.
"BAKWATA
imewataka wananchi wote kufuata taratibu sahihi jambo lolote linapo
tokea."Kama yupo mtu yoyote ana manung'uniko au hoja yoyote dhidi ya
mwenzake au taasisi yoyote,ni lazima watumie taratibu sahihi za kidini
au za kisheria na sio kuchukua sheria mkononi"alisema Sheikh Issa.
Alisema baraza hilo linamuomba Mwenyezi Mungu awaponye watu wote waliathirika na tukio hilo.
.............................................................................
RAIS DKT. KIKWETE APOKEA ZAWADI YA JEZI NAMBA 10 KUTOKA BARCELONA, ANAYOVAA NGULI MESSI KUTOKA!!
Rais
Dktk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mpenzi mkubwa wa michezo amepewa zawadi
ya Jezi namba 10 ya mwanasoka bora wa FIFA mara nne mfululizo,
mshambuliaji wa Barcelona, Raia wa Argentina, Lionel Andrew Jorge Messi
No comments:
Post a Comment