Mwari huyo!: Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya likiwa limewekwa  Nyon, Switzerland wakati wa droo mchana huu
 DROO YA ROBO FAINALI IMEMALIZIKA HIVI
Barcelona vs Atletico Madrid
Real Madrid vs Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain vs Chelsea
Manchester United vs Bayern Munich
Mechi za kwanza zitachezwa mwezi wa nne tarehe 1 na 2, wakati mechi za marudiano zitapigwa mwezi wa nne tarehe 8 na 9.
David
 Moyes alifuzu kwa juhudi kubwa baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi 
ya  Olympiacos  dimba Old Trafford ambapo mechi ya kwanza nchini Ugiriki
 alipigwa 2-0. Lakini sasa amepewa kazi nyingine ngumu zaidi kama 
anataka kufuzu nusu fainali.
Moyes
 ambaye bado yupo katika msongo wa mawaza kufuatia kipiga cha 3-0 kutoka
 kwa Liverpool wiki iliyopita, atakutana na kocha wa zamani wa 
Barcelona, Pep Guardiola ambaye sasa yupo Allianz Arena.
Bayern
 ambao waliwatupa nje Man United mwaka 2010 walikuwa wa kwanza katika 
kundi lao lililokuwa na klabu za Manchester City, CSKA Moscow na 
Viktoria Plzen.
Amefurahi?
 Samuel Eto’o na Chelsea yake wameliwatoa  Galatasaray baada ya 
kuwafumua mabao  2-0  uwanjani  Stamford Bridge hatua ya 16.
 Vijana wakubwa: Nyota wa Real Madrid,  Cristiano Ronaldo (kulia) na Gareth Bale wanatafuta kombe lingine
 Mabingwa watetezi!: Bayern Munich walifuzu robo fainali baada ya kuwalowesha Arsenal
Usitusamehe: Lionel Messi na Barcelona yake waliwatungua  Manchester City na kufuzu robo fainali
 
 
 
No comments:
Post a Comment