TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 27.04.2014.
- MTOTO WA MIAKA MITATU AUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI.
- MTOTO WA MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 MTOTO
 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA PATRICK NJOJO (03) MKAZI WA ISISI, 
WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE 
PATRICK  NJOJO (23) MKAZI WA ISISI.
 TUKIO
 HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 23:45 USIKU HUKO 
KATIKA KIJIJI CHA ISISI, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, 
MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA 
KIENYEJI WA BABA HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU 
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBARALI.
 KAMANDA
 WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED 
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA 
ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI 
KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.
 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MTOTO
 MWENYE UMRI WA MIAKA 4 – 5 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO  MBIGA, 
MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI 
LENYE NAMBA ZA USAJILI SM 9124 AINA YA FAW LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA 
DEREVA RAMADHANI MWALYOYO (30) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.
 TUKIO
 HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO 
KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA KUU
 YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA,
 MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA 
AMEKAMATWA.
 KAMANDA
 WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED 
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA 
MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
 KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
                                                      Signed by:
                                      [AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 
 
 
No comments:
Post a Comment