Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali
ya Mtaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo. Kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara za Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi
wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Denis Bandisa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (Tamisemi), Jumanne Sagini (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara za Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi
wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Denis Bandisa, akiwaonesha wanahabari
daftari la kura wakati akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo kuchukua taarifa hiyo.
Na -Dotto Mwaibale
WAKATI
wananchi wakijishauri kujiandikisha katika uchaguzi wa serikali za
mitaa, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi ) imekiri kuzorota kwa zoezi hilo,na hivyo kuwataka wananchi
kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
Akizungumza
na waandishi wahabari Dar es salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Jumanne Sagini alisema kuzorota huko kumetokana na serikali kuchelewa
kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kusababisha kukosa muelekeo.
Alifafanua
kuwa kwa kawaida uchaguzi huo hufanyika mwezi oktoba na hivyo waziri
mkuu anatakiwa kutoa taarifa hiyo siku 30 kabla lakini kutokana na
kuwepo kwa bunge lakatiba hali hiyo ilibadilika na hivyo kuiilazimu
serikali kusogeza mbele mchakato huo.
“Nikweli
hali hiyo ipo kama mnavyosema wandishi,lakini nyie ndio mnatakiwa
kutusaidia kuzidi kutoa elimu,tumekuwa tukifanya vipindi katika vyombo
mbalimbali vya habari lakini bado elimu inahitajika zaidi”alisema.
“Na wiki
ya kwanza jambo hili lilionekana kuzorota kwa sababu ilikuwa ni wiki ya
wagombea kuchukua fomu,wananchi wakajua ni siku ya kujiandikisha,lakini
mchakato unakwenda vizuri kwasiku hizi mbili”aliongeza.
Sagini
alipoulizwa na wandishi kuhusu mkanganyiko wa vituo vya kupigia kura
alisema vituo vyoye vilivyopo katika mazingira ya huduma za Afya
zinatakiwa kuondolewa na kupelekwa kwenye shule za msingi ilikuepusha
usumbufu kwa kwa wagonjwa.
kauli
hiyo ilitokana na kuwepo kwa kituo cha Zahanati ya Tandale kugeuzwa kuwa
kituo cha uandikishaji kwa wapiga kura hali inayopeleka wagonjwa
kulalamika kuwa wanapata usumbufu,hivyo kuwataka wahusika kuhamisha
kituo hicho.
Akizungumzia
bajeti ya uchaguzi huo, Mratibu wa uchaguzi Taifa, Denis Bandisa
alisema serikali imetenga bilioni 20 kwa ajili ya uchaguzi huo
ambapo,kati ya hizo bilioni nane kwa ajili ya malipo ya makarani,bilioni
sita vifaa vya kujiandikishia,na bilioni sita kwa ajili ya matumizi
mengine.
Hata
hivyo Denis hakutaka kubainisha kuwa matumizi mengine ni yapi katika
fedha hizo,na kusema kila karani atakuwa atalipwa sh. 10,000 kwa siku
kutokana bajeti ya serikali kuwa ndogo.
“Kipindi
cha mwanzo tlikuwa hatulipi kabisa,kwasababu sio kazi ngumu,ila kwasasa
tukaona sio vema kwa sababu wanatumia nauri zao,tukaamua kutenga kiasi
hicho cha fedha ila badae tutaangalia utaratibu wa kuwaongezea katika
uchaguzi mkuu”alisema Denis.
Hata hivyo alitaja idadi ya kata zinazo husika na uchaguzi kuwa ni 3,802,mitaa 3741,Vijiji 12,443 na vitongoji 64,616.
Hata hivyo gazeti hili lilipa baadhi ya vituo na kushuhudia makarani wakisema kuwa kwasiku huandikisha wananchi 30.
No comments:
Post a Comment