Mwezi mmoja uliopita KingoTanzania tumefanya mahojiano maalum na Chifu Jack Mwakibwili nyumbani kwake ambapo tumepata nafasi ya kujua Historia ya Rungwe katika nafasi za uongozi Uchumi, Utarii, pamoja na Mira na desturi za wanyakyusa
Lakin kwa kifupi Chifu mwakibwili baada ya uongozi wa kichifu kusitishwa na serikali yabawamu ya kwanza, Chifu Mwakibwili alikuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe, na katika uongozi wake ndiye aliyejenga jengo kubwa la mawe zuri na kuzinduliwa na Rais ambalo linatumika hadi Leo kama ofisi ya Halmashauri ya Rungwe.
Baada ya hapo akawa mbunge wa jimbo la Rungwe kwa miaka mitano, akiwa mbunge wa Rungwe alifanikiwa kusimamia ujenzi wa kituo cha afya kandete mwakaleli na masukulu na kuzinduliwa na waziri mkuu Marehem Sokoine.
Baada ya kuwatumikia wana Rungwe akapata nafasi ya kuwa mbunge wa mkoa wa mbeya kwa miaka kumi alipostafu ndipo akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Kyerucu na mafanikio ya majengo na Mali za Kyerucu zilizopo kama majengo zilizopo kyela na Rungwe basi ni wakati wa uongozi wa Chifu Mwakibwili.
Lakin Chifu mwakibwili ndiye chifu pekee aliyebaki hai kipindi hiki kati ya machifu kumi na mbili waliokuwepo wakati huo wa utawara wa kichifu
Wilaya ya Rungwe na mkoa wa mbeya na Taifa la Tanzania tuna kila sababu ya kujivunia Uwepo wa Chifu Mwakibwili kwan ni kati ya viongozi waadirifu, wanyenyekevu, wenye upendo na uchu wa maendeleowaliopata kuiletea sifa wilaya ya Rungwe na Taifa
Ni msiba mkubwa tuungane kumsindikiza Mzee wetu Chifu Mwakibwili. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana na lihimidiwe.
Amen
No comments:
Post a Comment