Monday, May 8, 2017

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AONGOZA MAMIA YA WATANZANIA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI, WALIMU NA DEREVA WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA BASI WILAYANI KARATU



Makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanja wa ndege jijini Arusha kwa ajili ya kuongoza tukio la kuaga miili ya wanafunza 33, walimu wawili na dereva katika uwanja wa Shekh Amri Abeid tukio ambalo linaendelea kwa sasa.



Mamia ya watanzania wajitokeza katika uwanja wa Shekhe Amri Abeid Jijini Arusha wakiongozwa na makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuaga miili ya wanafunzi 33 walimu wawili na dereva waliofariki katika ajali ya basi wilayani karatu mwishoni mwa wiki.

Picha ya pamoja ya wanafunzi thelathini na mbili, walimu wawili na dereva mmoja waliopoteza maisha katika ajali ya basi iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika mlima Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.


No comments: