Rais Jacob Zuma kufanya Ziara Tanzania, atawasili Jumatano kwa ziara ya siku tatu nchini.
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini,Jacob Zuma, anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia jumatano ijayo, huku masuala yanayohusu ushirikiano wa nchi mbili hizo, Biashara na uweekazaji pamoja na kikanda na kimataifa yakiwa ajenda muhimu ya mataifa hayo.
Ziara ya Rais Zuma wa Afrika kusini atakayeambatana na mawaziri sita na wafanyabiashara 80 itashuhudia mkataba wa uanzishwaji wa maeneo kumi ya ushirikiano katika sekta mbalimbali.
Waziri wa wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi AGUSTINO MAHIGA amewaeleza waandishi wa habari kuwa katika ziara hiyo mikataba kadhaa inatarajiwa kusainiwa ambapo miongoni mwake ni hati ya makubaliano ya ushrikiano katika masuala ya Bio Anuwai na uhifadhi, sekta ya maji, pamoja na sekta ya uchukuzi.
Katika ziara hiyo, Rais Zuma mbali ya kufanya mazungumzo na m wenyeji wake, kukutana na wafanyabiashara pia atafungua jengo jipya la ubalozi wa nchi hiyo pamoja na kutembelea taasisi ya matibabu ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Katika hatua nyingine Makatibu wakuu wa Afrika kusini na Tanzania wameanza mkutano wa siku mbili kujadili Tume ya Mashirikiano ya Marais ili kuainisha maeneo ya ushirikiano kabla ya wakuu hao kuhitimisha kwa kuweka saini.
Afrika kusini ni taifa la Pili kwa miradi ya mingi ya uwekezaji kibiashara nchini, ambapo imewekeza miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilion tano.
No comments:
Post a Comment