Rais Donald Trump wa Marekani amewahamasisha waungaji wake mkono jana kwa kutetea jibu lake la maandamano yaliyoandaliwa na kundi linalowaona wazungu kuwa jamii bora mjini
Virginia na kuahidi kusitisha utendaji wa serikali ikiwa ni lazima ili kujenga ukuta katika mpaka na Mexico. Akishutumiwa kwa kusema pande zote zilikuwa na makosa kutokana na ghasia zilizotokea katika maandamano hayo, Trump amevishutumu vituo vya televisheni kwa kupuuza wito wake wa umoja baada ya tukio hilo.
Polisi walitumia maji ya pilipili kuwatawanya waandamanaji baada ya kurusha mawe na chupa nje ya kituo cha mikutano ambako Trump alikuwa akihutubia. Trump alionya jana huenda akasitisha makubaliano ya kibiashara ya NAFTA na Mexico na Canada baada ya majadiliano ya pande tatu kushindwa kutatua tofauti zilizopo.

No comments:
Post a Comment